Angalia picha: TUNDU LISSU AIBUKA MKUTANO MKUU ACT- WAZALENDO


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu,  ameibuka ndani ya Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo.


Mkutano huo unafanyika leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Lissu aliingia ukumbini wakati Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo akijiandaa kutoa hotuba kwa wajumbe wa mkutano huo.

Kabla hajaanza, Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, akaingia ukumbini akiwa ameambatana na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar.

Kabla hajakaa katika nafasi iliyokuwa imeandaliwa, Zitto alimwita Lissu na Bernard Membe, Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo wapande jukwaani hali iliyoibua shangwe zaidi. 
Membe anatarajiwa kuteuliwa na mkutano huo kuwa mgombea urais



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527