STEPHEN MASELE ACHUKUA FOMU KUGOMBEA TENA UBUNGE SHINYANGA MJINI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 14, 2020

STEPHEN MASELE ACHUKUA FOMU KUGOMBEA TENA UBUNGE SHINYANGA MJINI

  Malunde       Tuesday, July 14, 2020


Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Julius Masele (kulia).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (2010 - 2020), Stephen Julius Masele amechukua fomu ya kuomba kugombea tena Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Stephen Julius  Masele amechukua fomu leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ambapo Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Mashema alikuwa anatoa fomu hizo kwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Masele amesema sababu kubwa ya kuomba ridhaa ya wanachama wa  CCM  kumptisha kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini ni kukamilisha na kuendeleza kazi za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambazo amezifanya katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post