MNEC GASPAR KILEO 'GAKI' AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINIKushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Gaspar Kileo (kulia).

Na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo maarufu 'GAKI' amechukua fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Gaspar Kileo amechukua fomu leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ambapo Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu alikuwa anatoa fomu hizo kwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Gaspar Kileo amesema atazungumzia vipaumbele vyake mara baada ya chama chake kumpitisha kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo akiwa ameshikilia fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu,kulia ni mtoto wa Gaspar, Kileo Gladness 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo akiwa ameshikilia fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu,kulia ni mtoto wa Gaspar, Kileo Gladness 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo akiwa ameshikilia fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post