KAULI YA STEVE NYERERE BAADA YA KUPATA KURA 6 IRINGA MJINI


“Kwanza nichukue nafasi hii kusema asante Mungu kwa kila jambo, hakika nimeona uwezo wako nimeona nguvu yangu nimeona kipaji changu nimeona jinsi gani Baba anavyonipigania kwenye kila jambo, niseme Asanteni sana Wasanii wenzangu mlionikimbilia kwenye hili.


“Asante marafiki zangu Ndugu zangu pamoja na Waandishi wa habari wote nasema bila nyie mimi siwezi, niseme asante kwa Chama changu Viongozi wote wa Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Ally Hapi, Salim Asas, DC Richard Kasesela na Viongozi na Wanachama wote wa CCM

“Niseme tu kukosa kura sio sababu ya kuacha mapambano nitashirikiana na Mgombea kuhakikisha Jimbo linarudi lakini kikubwa zaidi ni kutafuta ushindi wa hali ya juu wa Chama cha Mapinduzi kuanzia kura za Rais, Mbunge mpaka Diwani

“Narudia tena asante Iringa hakika nimejiona wa thamani sana tulikuwa Wagombea 57 katika hao wote mimi Steve Nyerere nimekuwa Mtu wa 9, wengine wote kura 1 wengine sifuri, hivi ningekosa kabisa ningeweka wapi sura yangu asante wana Iringa hata hichi kidogo mlichonipa kwangu ni heshima pia




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527