FREEMAN MBOWE, MCHUNGAJI PETER MSIGWA WAJITOA MCHAKATO WA KUGOMBEA URAIS CHADEMA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 20, 2020

FREEMAN MBOWE, MCHUNGAJI PETER MSIGWA WAJITOA MCHAKATO WA KUGOMBEA URAIS CHADEMA

  Malunde       Monday, July 20, 2020

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na makada wengine watatu  wamejiengua  katika kinyang’anyiro cha kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.


Wanachama hao walikuwa miongoni mwa 11 waliotia nia kuwania urais ndani ya chama hicho lakini hawakujitokeza kuchukua fomu pindi shughuli ya uchukuaji na urejeshaji ilipoanza tarehe 4 hadi 19 Julai 2020.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama cha Chadema, Rebby Munisi amesema watia nia waliochukua na kurejesha fomu ni Wakili Simba Neo, Aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Mchungaji Leonard Manyama, Dk.Maryrose Majinge, Wakili Gaspar Mwanalyela, Lazaro Nyalandu na makamu mwenyekiti wa chama hicho Bara, Tundu Lissu.

Miongoni mwa watia nia ambao hawakuchukua fomu za urais ni pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Nalo Opiyo na Msafiri Shabani.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post