ATUPWA JELA KWA KUMTUKANA MAMA YAKE INSTAGRAM | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 23, 2020

ATUPWA JELA KWA KUMTUKANA MAMA YAKE INSTAGRAM

  Malunde       Thursday, July 23, 2020
MKAZI wa Mbuyu Zanzibar, Daurat Salum Suleiman amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni tano au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumtusi mama yake mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Suleiman alihukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Ilala jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Martha Mpaze.

Hakimu Mpaze alisema upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi sita kuthibitisha mashitaka ya udhalilishaji kwa njia ya mtandao na kwamba wameweza kuthibitisha mashitaka hayo bila kuacha shaka lolote.

Alisema baada ya kusikiliza mashahidi wa alibaini maneno aliyoandika mshitakiwa yalikuwa na lengo la kumdhalilisha mlalamikaji Shabaha Said Chondoma maarufu kwa jina la teacher licha ya kwamba Suleiman alikataa kutenda kosa hilo wakati akijitetea.

"Baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi sita na vielelezo, mahakama inakutia hatiani kwa   kumdhalilisha kimtandao Chondoma hivyo, utatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano na akishindwa kulipa fedha hiyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela," alisema Hakimu Mpaze.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post