MWANDISHI HABARI JOSEPHINE CHARLES ATINGA HOSPITALI YA KOLANDOTO KUSHEHEREKEA 'BIRTHDAY' YAKE
Na Marco Maduhu -Shinyanga.

Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Matangazo Radio Faraja iliyopo mjini Shinyanga Josephine Charles, amesheherekea siku yake ya kuzaliwa katika hospitali ya Kolandoto iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.


Leo Julai 23, 2020 Mwandishi huyo Josephine Charles ametimiza miaka yake kadhaa ya kuzaliwa, ambapo ameamua kusheherekea na akina mama wajawazito, pamoja na akina mama ambao wamejifungua watoto wao siku ya leo kwenye hospitali hiyo ya Kolandoto.

Amesema tangu mwaka jana amekuwa na kawaida ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa hospitalini, ambapo mwaka huo alisheherekea na akina mama waliojifungua watoto katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, pamoja na kutoa zawadi mbalimbali.

"Leo nimeamua kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa na akina mama wajawazito pamoja na akina mama ambao wamejifungua watoto wao katika hospitali hii ya Kolandoto, pamoja na kula nao keki na kuwapatia sabuni za kufulia, kuogea pamoja na mafuta ya watoto wachanga," amesema Josephine.

"Pia natoa wito kwa wajawazito mkoani Shinyanga wajenge utamaduni wa kujifungulia watoto hospitalini maeneo ambayo ni salama, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi," ameongeza.

Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Kolandoto Zephania Msunza, amempongeza mwana habari huyo kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na wajawazito na akina mama waliojifungua watoto, na kubainisha kitendo hicho kinapaswa kuigwa, na siyo kwenda kufanya anasa ikiwamo kunywa pombe.

Amesema watu wengi wangekuwa wakisheherekea siku zao za kuzaliwa hospitalini, changamoto nyingi za uhaba wa vifaa ingepungua, na kutoa wito kwa wengine kufanya hivyo ili kuboresha huduma za kiafya.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Josephine Charles akikata keki.


Muonekano wa keki.

Josephine Charles akimlisha keki mama mjawazito katika hospitali ya Kolandoto kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Zoezi la kula keki likiendelea.

Zoezi la kula Keki likiendelea.

Zoezi la kula keki likiendelea.
Josephine akimlisha keki mganga mfawidhi wa hospitali ya Kolandoto Zephania Msunza.

Josephine akimlisha keki muuguzi mfawidhi wa hospitali ya Kolandoto Christina Richard.

Josephine Charles, kushoto akimlisha Keki mfanyakazi wenzake wa Radio Faraja Jackline Januari.

Zoezi la kula keki likiendelea.Mganga mfawidhi wa hospitali ya Kolandoto Zephania Msunza, kulia, akimlisha Keki Josephine Charles.

Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.

Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.

Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.

Awali mwandishi wa habari kutoka kituo cha Matangazo Radio Faraja mjini Shinyanga Josephine Charles, wa pili kutoka kushoto akiwasili na baadhi ya wafanyakazi wenzake kusheherekea siku yake ya kuzaliwa katika hospitali ya Kolandoto.

Josephine Charles wa kwanza kushoto akiimbiwa nyimbo ya Happy birthday.

Josephine Charles (wa tatu kutoka kushoto), akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake pamoja na mganga mfawidhi na muuguzi mfawidhi katika hospitali ya Kolandoto mara baada ya kumaliza kusheherekea siku yake ya kuzaliwa hospitalini hapo.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post