WALIOKUWA VIONGOZI WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA RUKWA MATATANI TENA


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Rukwa Hamza Mwenda amekabidhiwa ripoti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) nchini na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ili kuyashughulikia yaliyomo ndani ya ripoti hiyo na kuwakama wote waliohusika na ubadhirifu wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani humo.

Mh. Wangabo amesema kuwa ripoti hiyo imetokana na uchunguzi uliofanya na COASCO mapema mwaka huu ili kubaini ubadhirifu uliofanywa na uongozi wa chama hicho cha Ufipa Co-operative Union (UCU) baada ya viongozi hao kuingia mkataba na kampuni ya pembejeo ya Eli Agrovent Co, ili kununua mbolea jambo katika mchakato wa manunuzi ya mbolea hiyo kiasi cha Shilingi milioni 277 zilipotea.

“COASCO walifanya ukaguzi wa kina kuanzia mwezi Machi na wakatoa taarifa ndani ya Mwezi huo huo mwaka huu 2020, na kubaini kwamba kuna mapungufu mengi yakiwemo ubadhirifu wa hawa viongozi waliokaa ndani ya miezi sita tu, hawa viongozi wa chama cha ushirika cha Ufipa (UCU), TAKUKURU nakukabidhi ripoti hii ya COASCO Mkaishughulikie kwa kina, na wale wote waliohusika kufanya ubadhirifu wakamatwe, warejeshe, fedha zirudishwe, nakukabidhi ripoti.”

“Hawa wote walioko hapa wameteswa na viongozi wa vyama vya ushirika, na watesaji bado wapo, fedha zimeokolewa kutoka kwa watu ambao hawakufuata sheria ya vyama vya ushirika na kanuni zake, wakawatesa hawa kwahiyo waliowatesa wapo na wenyewe wapate mateso yanayostahiki,” Alisisitiza.

Na kuongeza kuwa wanachama wengi wamekuwa wakisita kujiunga na vyama hivi kutokana na ubadhirifu unaofanywa na viongozi hao na hivyo kuogopa kujiunga na hivyo kumuagiza Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani humo pamoja na maafisa ushirika katika halmahsuri za mkoa huo kuhakikisha wanawapekuwa viongozi wote wabovu na kuwaondoa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527