TPDC YAZINDUA ENEO LA MRADI WA MAGHALA MAFUTA NA GESI DODOMA


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Patrobas Katambi,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zinje Kata ya Zuzu wakati akizindua Mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi uliozinduliwa na TPDC katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zinje Kata ya Zuzu ambao wamepisha eneo la ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi mradi uliozinduliwa na TPDC katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,Dkt.James Mataragio,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zinje Kata ya Zuzu ambao wamepisha eneo la ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi mradi uliozinduliwa na TPDC katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
Meneja wa Tanoil,Mhandasi Kapuulya Musomba,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zinje Kata ya Zuzu ambao wamepisha eneo la ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi mradi uliozinduliwa na TPDC katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw.George Seni,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zinje Kata ya Zuzu ambao wamepisha eneo la ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi mradi uliozinduliwa na TPDC katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Zuzu Bw.Omari Bilali,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma,Mradi huo umezinduliwa na TPDC.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Pinda Bw.Salvatory Olesaitabau ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma,Mradi huo umezinduliwa na TPDC.
Mtendaji wa Kata ya Zuzu Bw.Mabrouk Seif,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma,Mradi huo umezinduliwa na TPDC.
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Zinje Kata ya Zuzu ambao wamepisha eneo la ujenzi wa mradi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi Mkoani Dodoma,Mradi huo umezinduliwa na TPDC.
Bw.Juma Boniphace moja Kati ya wananchi wa Kijiji cha Zinje Kata ya Zuzu ambao wametoa maeneo yao kupisha ujenzi wa Mradi, akitoa Shukrani kwa niaba ya wananchi wenzeke.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akikabidhi mfano wa hundi kwa malipo ya fidia kwa wananchi wa Kijiji cha Zinje Kata ya Zuzu waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi wa mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Patrobas Katambi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi uliozinduliwa na TPDC katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde,akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,Dkt.James Mataragio mara baada ya uzindua Mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mafuta na gesi uliozinduliwa na TPDC katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
…………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi Wetu, Dodoma 

TPDC imezindua eneo la mradi wa kujenga maghala ya kuhifadhia Mafuta na gesi katika eneo la Zuzu mkoani Dodoma. 

Uzinduzi huo umefanyika leo baada ya kukamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi 19 ambao wamelipwa zaidi ya shilingi milioni 128 kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa mradi wa kujenga maghala ya kuhifadhia Mafuta na gesi katika eneo la Zuzu uliyozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobasi Katambi. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt.James Mataragio amesema kuwa shughuli za TPDC ni utafutaji , usambazaji na uuzaji wa Nishati ambayo ni gesi asilia na Mafuta.

 “Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha nishati inawafikia wananchi wote ili kuunga juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda”, ameeleza Dkt. Mataragio .

 Aidha Dkt. Mataragio amesema kuwa kufikia uchumi wa viwanda lazima kusambaza nishati ya uhakika ili kuleta matokeo chanya kwa wanachi kufikia adhima ya uchumi wa viwanda. 

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amesema kuwa ujio wa mradi wa kujenga maghala ya kuhifadhi Mafuta na gesi utafungua wigo mpana kwa wakazi wa eneo hilo katika kuleta maendeleo . 

“Napenda kuwa pongeza wanachi wote wa eneo hili kwa uzalendo wenu wa kutaka kupata maendeleo kwa kupisha mradi huu katika eneo hili kwa kutaka mradi huu kutekelezwa kikamilifu ili kuleta maendeleo”, amesema Katambi. 

Katambi ameongeza kuwa kitendo cha kupisha mradi huu kutekelezwa katika eneo hilo wakazi wa hapo watapata ajira,wamelipwa fidia, barabara zitajengwa na mzunguko wa pesa utaongezeka katika eneo hili hivyo wakazi wahapo wametakiwa kuutunza mradi huo ili kupata matokeo chanya kupitia mradi huo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amewataka Wakazi wa eneo hilo kutumia fedha za fidia walizolipwa na Shirika la Maendeleo ya Petro Tanzania kuboresha maisha yao kwa kujenga vitega uchumi vitakavyowasaidia kuwaletea maendeleo.

Meneja Mkuu wa Tan Oil, Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kuwa baada ya zoezi la kupata ardhi kukamilika sasa hataua inayofata ni kurasimisha eneo hilo liweze kupatiwa hati alafu upembuzi ya kinifu utafanyika kwa ajiri ya kuanza kutekeleza mradi huo. 

Kwa upande wake
Bw.Juma Boniphace mmoja wa wakazi wa Kata ya Zuzu ambaye amepisha ujenzi huo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake amesema kuwa wao kama wakazi wa Zuzu wanashukuru sana kwa wahusika na serikali kwa ujumla kuwaletea maendeleo na baada ya mradi huo kukamilika zuzu itabadilika sana kimaendeleo na wao wako tayari kuendeleza maendeleo hayo yatokanayo na mradi huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527