Mwakyembe Apongeza Wazalendo Wanaounga Mkono Juhudi za Rais Magufuli

Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa pongezi kwa Wazalendo wanaounga mkono juhudi za Dkt.John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kazi aliyo nayo katika kuliletea Taifa Maendeleo.

Dkt.Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo Jijini Dodoma alipopokea kitabu kinachoitwa “Rais Magufuli Kusudi la Mungu” kilichoandikwa na Bi.Eva Kaaya  Diwani wa Viti Maalum (CHADEMA) katika Halmashauri ya Meru Arusha ambacho kimeelezea utashi wa Mhe. Rais kwa wananchi wake katika kuwaletea maendeleo ambayo yameonekana tangu  alipoingia madarakani.

“Kitabu hiki kimebeba maono ya Mkuu wetu wa nchi, nimekisoma kwa muda mfupi lakini nimeona jinsi ulivyodadavua utekelezaji wa Awamu hii ya Tano kwa wananchi wake, na hii ni kutokana na msimamo wake katika kipindi cha kupambana na ugonjwa wa Covid-19 ambao umepelekea Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kusamehe madeni ya nchi yetu”, alisema Dkt.Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa juhudi za Mhe. Magufuli katika Sekta anazosimamia  zimeonekana ikiwemo mafanikio katika soka na matumizi ya lugha ya Kiswahili na kulinda mila na desturi ambazo ndio utambulisho wa nchi.

Kwa upande wake, Mwandishi wa kitabu hicho, Bi. Eva Kaaya amesema lengo la kuandika kitabu hicho ni kuieleza jamii kusudi la Mungu kwa Mhe. Rais Magufuli kwa watanzania ambapo ameongeza kuwa Mhe.Rais anapaswa kuungwa mkono na watanzania wote.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwakyembe ameeleza aziama ya serikali ya kuboresha Uwanja wa ndani ili utumike katika michezo mbalimbali wakati huu mchakato wa kuanza ujenzi wa Arts and Sports Arena ukiendelea.

Dkt. Mwakyembe amesema hayo baada ya kukutana na mtoto Romeo Asubisye aliyeshinda medali takriban tisa katika mashindano ya kuogelea kwa nchi mbalimbali ambaye ameeleza changamoto ya mabwawa  ya kuogelea hapa nchini, ambapo ameeleza kuwa uhitaji wa mabwawa ya kuogelea ni yenye urefu wa mita 50 na mengi yaliyopo ni mita 25.

Kwa upande wake mtoto Romeo Asubisye  ameiomba Serikali kuwekeza katika mchezo wa kuogelea kwa kuwezesha upatikanaji wa mabwawa, makocha pamoja na wataalam wazidi ili mchezo huo ukue hapa nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments