PROF. PALAMAGAMBA KABUDI 'AUTAKA UBUNGE' KILOSA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 29, 2020

PROF. PALAMAGAMBA KABUDI 'AUTAKA UBUNGE' KILOSA

  Malunde       Monday, June 29, 2020

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Prof. Palamagamba Kabudi amesema yupo tayari kuwatumikia wananchi wa jimbo la Kilosa iwapo watamhitaji kwenda kufanya hivyo.


Kabudi ameonyesha nia hiyo leo tarehe 29 Juni 2020 wilayani Kilosa, wakati akihutubia katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa mahandaki manne yenye urefu wa kilomita 2.7 ya reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Makutupora.

Licha ya kwamba hakutaja hadharani nia ya kugombea ubunge Kilosa, Profesa Kabudi amesema, kama atapata kibali kutoka kwa Mungu, hatakataa kuwa mtumishi wa wananchi wa Kilosa.


“Mimi ni kijana wenu, mzaliwa wa hapa na niwaambie kuwa mkinihitaji kuwatumikia niko tayari” amesema Kabudi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post