NCCR- MAGEUZI WATANGAZA RATIBA YA MCHAKATO WA UCHAGUZI


Chama cha NCCR-Mageuzi kimetangaza ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu katika chama hicho kuanzia leo hadi Julai 8 mwaka huu.


Akitangaza ratiba hio, Katibu Mkuu wa chama hicho, Elizabeth Mhagama amesema kuwa fomu ya kugombea urais itatolewa katika Makao Makuu ya chama hicho huku fomu za ubunge na udiwani zikitolewa katika kata na majimbo husika.

“Kwa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watachukua  fomu hapa Makao Makuu itatolewa na Katibu Mkuu, kwa wagombea urais Zanzibar watachukua fomu hizo katika halmashauri kuu maalum iliyopo Zanzibar huko yupo Naibu Katibu Mkuu Zanzibar vile vile kwa wawakilishi” amesema Mhagama

NCCR-Mageuzi  imetangaza ratiba hiyo wakati ambapo vyama mbalimbali vimeshatangaza ratiba zao za kuchukua na kurejesha fomu ,sambamba na kutangaza nia kuwania nafasi mbalimbali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527