Picha : DC SHINYANGA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amefungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) uliolenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu Klabu hiyo na Tasnia ya Habari mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika leo Jumamosi Juni 13,2020 katika Ukumbi wa Liga Hoteli Mjini Shinyanga, Mhe. Mboneko aliwapongeza Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano mkubwa walionao pamoja na mahusiano mazuri waliyonayo kwa wadau wa habari mkoani humo.

“Waandishi wa habari mmekuwa wadau wakubwa wa maendeleo. Hata tunapowaita mmekuwa mkijitokeza kuihabarisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali”,alisema Mboneko.

“Nawapongeza pia kwa kuanzisha Blogu ‘Shinyanga Press Club Blog’ na kuwa karibu na wadau wa habari kwa kuanzisha Group la Whatsapp ambalo linajumuisha pia viongozi wa serikali na wadau mbalimbali ili kupeana taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitusaidia pia kutekeleza majukumu yetu na kujua mambo yanayoendelea katika jamii”,alieleza Mboneko.

Katika hatua nyingine, Mboneko aliwataka waandishi wa habari kuandika habari zenye kulinda amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Mkuu huyo wa wilaya aliwashauri waandishi wa habari kuanzisha miradi ya maendeleo ili kujipatia kipato ikiwa ni pamoja na kutumia fursa zilizopo katika wilaya ya Shinyanga na mkoa kwa ujumla.

“Naomba pia muanzishe Timu ya Mpira wa miguu na pete. Nitafurahi sana siku nikiona Timu ya waandishi wa habari ikicheza na Timu ya Maveterani. Mazoezi ni muhimu kwa afya. Na nimetoa nafasi 10 kwa waandishi wa habari Shinyanga kushiriki mafunzo ya Jeshi la Akiba ambayo yatafanyika hivi karibuni”,alisema.

Aidha Mboneko aliwataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kujiendeleza kielimu ili kuendana na Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inayomtaka kila mwandishi wa habari awe na Diploma.

Mkuu huyo wa wilaya ametumia fursa ya Mkutano huo kuisaidia Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Lita 10 za sabuni ya kunawia mikono ili kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde alisema Klabu hiyo ni mdau mkubwa wa Maendeleo katika mkoa huo na inaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tunawashukuru wadau kwa kuendelea kufika katika ofisi ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.Takwimu zinaonesha kuwa kati ya mwaka 2017 hadi Mei 2020, Jumla ya wadau 426 kati yao wanaume 329 na wanawake ni 97 wamefika katika Ofisi ya waandishi wa habari SPC kwa Mahitaji ya huduma ya vyombo vya habari, ushauri,kusalimia, kujitambulisha na kutambulisha shughuli wanazofanya, kutoa taarifa za matukio,wananchi wenye mahitaji maalumu kuunganishwa kwa viongozi wa serikali na sekta binafsi",alisema Malunde



Licha ya wadau kuwa na mwamko mkubwa kuhusu umuhimu wa vyombo vya habari, Bado kuna changamoto ya uwepo wa baadhi ya sheria katika tasnia ya habari ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari mwaka 2016, Sheria ya Takwimu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015 na Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018 ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao”,alisema Malunde.

“Nawasihi waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kufuata sheria za nchi hasa katika kipindi hiki cha Mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Tutumie kalamu zetu vizuri kulinda Amani ya Nchi Yetu”,aliongeza Malunde.

Malunde alimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Limited, ndugu Salum Hamis kwa kufadhili Mkutano Mkuu wa Wanachama wa SPC 2020 kwa kuwapatia vinywaji baridi  ‘Jamukaya Soda,Maji na Juisi’.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kulia) akipokelewa na Viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) katika Ukumbi wa Liga Hoteli Mjini Shinyanga kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) uliolenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu Klabu hiyo na Tasnia ya Habari mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 13,2020. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa SPC, Kadama Malunde. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa SPC, Ali Lityawi akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa SPC, Shaban Alley -  Picha zote na Shinyanga Press Club
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kulia) akipokelewa na Viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) katika Ukumbi wa Liga Hoteli Mjini Shinyanga kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kulia) akiwasalimia waandishi wa habari alipowasili katika ukumbi wa Liga Hoteli kufungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC).Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa SPC, Kadama Malunde.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC). Kulia ni Mwenyekiti wa SPC, Kadama Malunde, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa SPC, Shaban Alley.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC). Wa kwanza kushoto ni Mweka Hazina wa SPC, Stella Ibengwe akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa SPC, Shaban Alley. Wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji wa SPC,Ally Lityawi akifuatiwa na Mwenyekiti wa SPC, Kadama Malunde.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC).
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwahamasisha waandishi wa habari kuandika habari zenye kulinda amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Kwa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa SPC, Kadama Malunde.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Kadama Malunde  akisoma taarifa ya Klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Kadama Malunde  akisoma taarifa ya Klabu hiyo.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Kadama Malunde msaada wa sabuni ya kunawia mikono ili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona katika Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Kadama Malunde msaada wa lita 10 za sabuni ya kunawia mikono ili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona katika Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa SPC, Shaban Alley akitoa neno la shukrani baada ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kufungua mkutano Mkuu wa wanachama wa SPC.
Awali Katibu Mtendaji wa SPC,Ally Lityawi akitambulisha wajumbe wa mkutano mkuu wa wanachama SPC
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC). 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC). 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na Wajumbe Kamati Tendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC).
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na Mwenyekiti wa  Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC),Kadama Malunde (kulia) na Katibu wa SPC, Ali Lityawi ( wa kwanza kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa SPC, Shaban Alley. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimweleza jambo Mwenyekiti wa  Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC),Kadama Malunde baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Wanachama SPC 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimweleza jambo Mwenyekiti wa  Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC),Kadama Malunde baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Wanachama SPC 2020.
Mwenyekiti wa  Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC), Kadama Malunde akiongoza Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji wa SPC Ally Lityawi. Wa kwanza kushoto ni Mweka Hazina wa SPC  Stella Ibengwe akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa SPC, Shaban Alley.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakisoma taarifa mbalimbali za Klabu hiyo
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
MC wakati wa mkutano Mkuu wa wanachama wa SPC, Mwandishi wa  Radio Kwizera, Amos John maarufu 'MC Mzungu Mweusi' akiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527