WAZIRI JAFO AZINDUA MRADI WA BARABARA KIGOMA UJIJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo akizundua barabara ya km 12 ya zaidi ya Sh bilioni 18 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji leo.

Na Moureen Tesha - Kigoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo amezindua mradi wa barabara wenye zaidi ya thamani ya bilioni 18 katika manispaa ya Kigoma Ujiji, uliojengwa chini ya mradi wa uendeshaji wa miji na majiji kimkakati Tanzania TSCP kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Akizindua mradi huo hii leo Alhamis Juni 4,2020 Waziri Japo amesema lengo la serikali ni kuhakikisha miji na majiji kote nchini inabadilika kwa kujengwa kwa kiwango cha lami bora, na kuweka taa za kisasa huku akiridhika mradi huo kwa namna ulivyo jengwa kwa lami ya kisasa na nzito.


Jafo amesema barabara hizo za Manispaa ya Kigoma Ujiji ni miongoni mwa barabara zinatekelezwa katika miji nane nchini akiwemo Mwanza,Dodoma, Mtwara, Tanga,Arusha kwa fedha za mkopo nafuu zaidi ya dola za kimarekani Milioni 343 sawa na zaidi ya Sh bilioni 800.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amewataka wananchi kuboresha mazingira ya makazi ili kuendana na hali ya mji ulivyo kwa sasa ambapo wakazi wengi huishi kwenye nyumba za majini jambo ambalo amekuwa akilikemea mara kwa mara.

Nao wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji wamepongeza hatua ya serikali kujenga barabara hizo za kiwango cha lami nzito na kwamba shughuli za uzalishaji zimeongezeka ikiwemo za madereva bodaboda na bajaji, hatua ambayo imepunguza wimbi la uporaji mitaani.

Mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Maclena Paulo, amesema uwepo wa barabara hizo kumerahisisha usafiri na mizunguko ya wananchi.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na wananchi kabla ya  kuzindua barabara ya km 12 ya zaidi ya Sh bilioni 18 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527