POLISI WENGINE WATATU WASHITAKIWA KWA MAUAJI YA MMAREKANI MWEUSI GEORGE FLOYD | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 4, 2020

POLISI WENGINE WATATU WASHITAKIWA KWA MAUAJI YA MMAREKANI MWEUSI GEORGE FLOYD

  Malunde       Thursday, June 4, 2020

Mwanasheria Mkuu wa Minnesota, Keith Ellison ametangaza kuwa maafisa watatu wa Polisi waliokuwepo wakati George Floyd anakandamizwa shingoni hadi kufariki wamefunguliwa mashtaka.

Thomas Lane (37), J. Alexander Kueng (26) na Tou Thao (34) wameshtakiwa kusaidia mauaji ya daraja la pili. Mashtaka ya Afisa aliyemuwekea goti Floyd, Derek Chauvin yamebadilishwa na sasa anatuhumiwa kwa mauaji ya daraja la pili

George Floyd alifariki dunia baada ya Chauvin kumkandamiza na goti shingoni huku maafisa wengine wakishuhudia. Mara baada ya kifo chake, Polisi hao wote walifukuzwa kazi lakini Chauvin pekee alishtakiwa kwa mauaji

Baada ya wote wanne kushtakiwa, Mwanasheria wa familia ya Floyd, Benjamin Crump amesema hii ni hatua kubwa kuelekea kupata haki na wamefarijika kwamba uamuzi huo umetolewa kabla George hajazikwa


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post