IGP SIRRO AWAAGIZA WAKUU WA POLISI WA WILAYA KUSIMAMIA MIKUTANO WAKATI WA KAMPENI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 4, 2020

IGP SIRRO AWAAGIZA WAKUU WA POLISI WA WILAYA KUSIMAMIA MIKUTANO WAKATI WA KAMPENI

  Malunde       Thursday, June 4, 2020
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewaagiza Wakuu wa Polisi wa Wilaya OCDs kuhakikisha wanasimamia mikutano wakati wa kampeni ili iwe ya amani na utulivu.


IGP Sirro amesema hayo leo akiwa mkoani Simiyu wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika mkoa huo na kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo ambapo alisema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kusimamia uchaguzi na kwamba litaendelea kutoa elimu kwa wananchi ikiwa pamoja na kushirikiana ipasavyo na wadau wa uchaguzi.

Aidha, IGP Sirro amewapandisha vyeo askari wawili wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU mkoa wa Simiyu kutoa cheo cha konstebo wa Polisi na kuwa Koplo wa Polisi kutokana na umahili wao wa kutekeleza majukumu wanayopewa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post