IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA AKIWEMO JONATHAN SHANA WA ARUSHA


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amemhamisha Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Salum Hamduni kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana amehamishwa kwenda kuwa Afisa Mnadhimu shule ya Polisi Moshi.

Hayo yameelewza  leo Jumatano June 24, 2020  na  Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini SACP David Misime  wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.  

Aidha, Miseme amesema kuwa   IGP Sirro, amemhamisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu Bunge, Dodoma ACP Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro na nafasi yake inachukuliwa na ACP Andrew Satta ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Polisi Dodoma.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527