ZITTO KABWE, SELEMAN BUNGARA (BWEGE) NA VIONGOZI WENGINE ACT-WAZALENDO WAACHIWA KWA DHAMANA


Kiongozi wa ACT Wazalendo Mhe.Zitto Kabwe na Bwana Seleman Bungara (Bwege) na viongozi wengine 6 wameachiwa kwa dhamana baada ya hapo jana kukamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Lindi wakiwa katika kikao cha ndani Jimbo la Kilwa Kusini.


Zitto na viongozi hao walikamatwa jana Jumanne asubuhi tarehe 23 Juni 2020 wakiwa katika kikao cha ndani katika ukumbi wa Starnford Bridge, Kilwa Masoko mkoani Lindi.

Wengine ni; Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara maarufu ‘Bwege’ , Akida Mawanja, Mlinzi wa Zitto na Shaweji Mketo ambaye ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527