FELIX MKOSAMALI AHAMA NCCR- MAGEUZI NA KUTIMKIA CHADEMA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 18, 2020

FELIX MKOSAMALI AHAMA NCCR- MAGEUZI NA KUTIMKIA CHADEMA

  Malunde       Thursday, June 18, 2020

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Muhambwe Mkoani Kigoma kupitia Nccr-Mageuzi Felix Mkosamali, amekihama chama cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na  Chadema nakutangaza nia ya kuwania ubunge wa Jimbo la Muhambwe kupitia CHADEMA katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.“Nimehama chama cha NCCR-Mageuzi kwasababu kimekuwa kama kinyonga hakieleweki kipo CCM au upinzani, ni chama ambacho kimekuwa hakifanyi kazi yoyote ya kisiasa kwa miaka mitano sasa kimeanza kuweka wagombea kwenye majimbo ya Chadema,” amesema na kuongeza.

“Nimeona Chadema ndio chama sahihi kugombea ubunge kwasababu kuna wanasiasa wenye msiamamo wa kisaiasa na wenye kudai katiba mpya”.

Amesema kuwa amekihama chama hicho ili aendelee kupigania mambo ya msingi na si kujipendekeza na kuwa anaamini wanaohama vyama ni haki yao lakini wengi wanaitumia vibaya haki hiyo kwasababu ya njaa na kushibisha matumbo yao.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post