SERIKALI YAIFUNGIA TIMU YA JKT TANZANIA KUINGIA NA MASHABIKI


Serikali imezuia timu ya Jkt Tanzania  kucheza na mashabiki uwanjani katika mechi zake zote zilisosalia kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu huu, kutokana na kukiukwa kwa mwongozo wa Wizara Ya Afya michezoni.




Muongozo huo umekiukwa wakati wa mchezo dhidi ya klabu ya Yanga uliopigwa jana Juni 17, 2020 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Lorietha Lawrence, mashabiki walijazana sana uwanjani hivyo kukiuka kanuni inayoagiza kufuatwa muongozo wa umbali wa mita moja kutoka shabiki mmoja na mwingine.

Aidha taarifa hivyo imesisitiza vilabu wenyeji, wasimamizi wa michezo na wadau wengine kuendelea kusimamia kikamilifu muongozo wa Afya na taratibu nyingine ili kujikinga na maambukizi ya Covid-19.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527