ZITTO KABWE AWASILI MAHAKAMANI KUSIKILIZA HUKUMU YAKE HUKU TAYARI AKIWA AMESHANYOA KIPARA


Mbunge wa Kigoma ambaye ni Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amewasili Mahakamani pamoja na Mawakili wake, kusubiri hukumu dhidi ya kesi yake ya uchochezi huku akiwa tayari ameshanyoa kipara.Hukumu hiyo ya kesi ya uchochezi, inayotarajiwa kuvuta hisia za watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, itatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Kesi hiyo iliyofunguliwa tarehe 2 Novemba 2018 na Jamhuri, itahitimishwa leo kwa Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, ama kutupwa gerezani, kupigwa faini, au kuachiwa huru

Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Chama cha ACT –Wazalendo, alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527