WHO: AFRIKA HUENDA IKAATHIRIKA ZAIDI NA VIRUSI VYA CORONA


Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kwamba bara la Afrika huenda likawa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona. 



WHO inabashiri kuwa hali ikiendelea ilivyo sasa, huenda idadi ya vifo ikafikia 300,000 na watu wengine zaidi ya Milioni 30 kuwa masikini.

Kufikia sasa Afrika ina vifo karibu elfu moja vinavyohusishwa na Corona, huku watu zaidi ya elfu 19 wakiambukizwa ugonjwa huo.

Wakati huo huo Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, limetaka Afrika isaidiwe kukabiliana na ugonjwa hatari wa Covid-19.

IMF imetoa wito wa msaada wa haraka wa kimataifa kwa nchi za Afrika ambazo zinakabiliwa na janga hilo.

Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva amewaambia mawaziri, maafisa wa Umoja wa Mataifa na wengine kwamba bara la Afrika halina raslimali za kutosha na miundo mbinu ya kutosha ya afya ili kukabiliana na janga hilo na kwamba linahitaji karibu dola bilioni 114.

Maambukizi ya virusi vya Corona kote ulimwenguni sasa yamepindukia milioni 2.18 na watu 150,000 wamepoteza maisha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527