IDADI YA MAAMBUKIZO YA CORONA MAREKANI YAPINDUKIA LAKI SABA


Idadi ya watu waliombukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imepindukia laki saba huku idadi ya wanaoaga dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 ikiongezeka kwa kasi nchini humo.

Takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa, watu 710,272 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani huku 37,175 wakiaga dunia na kuifanya nchi hiyo kuwa ndio iliyoathiriwa zaidi na virusi hivyo duniani.

Italia inashika nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya watu walioaga dunia kwa virusi vya Corona ambapo hadi sasa watu 22,745 wamefariki dunia nchini humo, ingawa kwa upande wa idadi ya maambukizo inashika nafasi ya tatu. 

Uhispania yenye idadi 20,002 ya vifo vya Corona, jumla ya watu 190,839 wameambukizwa virusi vya Corona katika nchi hiyo ya bara la Ulaya.

Nchi zinazofuata ni Ufaransa, Ujerumani na Uingereza na kulifanya bara la Ulaya kwa sasa kuwa kitovu cha virusi vya Corona.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527