WAZIRI MKUU WA UINGEREZA BORIS JOHNSON APELEKWA ICU BAADA YA HALI KUWA MBAYA KWA VIRUSI VYA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, April 7, 2020

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA BORIS JOHNSON APELEKWA ICU BAADA YA HALI KUWA MBAYA KWA VIRUSI VYA CORONA

  Malunde       Tuesday, April 7, 2020

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepelekwa katika chumba cha kuhudumia wagonjwa mahututi ICU baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya kwa siku kumi zaidi kwasababu ya ugonjwa wa virusi vya Corona, kwa mujibu wa msemaji katika makazi ya Waziri Mkuu.

 

Johnson amemuambia Waziri wa mambo ya nje Dominic Raab kuchukua usukani pale ambapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

Waziri Boris ,mwenye umri wa miaka 55, alilazwa katika hospitali ya St Thomas mjini London wakati hali yake ya kiafya ilipokuwa haina ahueni huku homa na kukohoa kukiongezeka zaidi siku ya Jumapili. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya ushauri kutoka kwa timu yake ya matibabu na anaendelea kupata huduma stahiki.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post