WAGONJWA WA CORONA KENYA WAFIKA 320....NI BAADA YA WENGINE 17 KUONGEZEKA


Wizara ya Afya nchini Kenya imesema idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona sasa imefika 320 baada ya leo kutangaza visa vipya 17, vilivyotokana na sampuli 668 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.Kati ya hao, 12 ni kutoka miji ya Mombasa na 5 Nairobi. 


Katibu Mkuu  Wizara ya Afya Nchini Kenya  Dkt. Mercy Mwangangi amesema wagonjwa 15 walichukuliwa na maafisa wa afya baada ya kuambatana na wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa awali huku hao 2 wakiwa ndani ya karantini. 

Wakati huo huo, Kenya pia imethibitisha kwamba wagonjwa 6 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha idadi ya waliopona nchini humo kufikia 89.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post