MWILI WA MWANAHARAKATI JOSEPHAT TORNER KUZIKWA KESHO IMALAMATE BUSEGA SIMIYUWaombolezaji wakibeba Jeneza lililobeba mwili wa Josephat Torner


Josephat Torner enzi za uhai wake

Mazishi ya Mwili wa Mwanaharakati wa kutetea Haki za watu wenye ualbino Josephat Torner Nkwabi (42) yanatarajiwa kufanyika kesho Alhamis Aprili 16,2020 katika kijiji cha Mwamwenge kata ya Imalamate wilaya ya Busega mkoani Simiyu alikozaliwa.

Josephat Torner Nkwabi amefariki dunia Siku ya Sikukuu ya Pasaka Aprili 12,2020 majira ya saa mbili usiku baada ya kugongwa na Hiace 'Daladala' akivuka barabara jijini Mwanza .

Mwili wa marehemu Josephat Torner ulikuwa unahifadhiwa katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza tangu Aprili 12,2020 ambapo leo Jumatano Aprili 15,2020 umesafirishwa kwenda wilayani Busega kwa ajili ya mazishi kesho.

Josephat Torner alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na Utetezi wa haki za Watu wenye Ualbino iitwayo Foundation of Josephat Torner Europe Aid (FOJOTEA) awali ikijulikana Josephat Torner Foundation Europe lakini pia amewahi kuwa Afisa Mahusiano na Habari wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS).

Josephat Torner Nkwabi alizaliwa tarehe 15.04.1978 na kufariki dunia tarehe 12.04.2020 siku tatu kabla ya Kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa kwake.

R.I.P Josephat Torner Nkwabi

Mwili wa Marehemu Josephat Torner ukiwa katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza leo Jumatano Aprili 15,2020

Mwili wa Marehemu Josephat Torner ukitolewa katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza leo Jumatano Aprili 15,2020 kwa ajili ya kusafarishwa kwenda wilayani Busega kwa ajili ya mazishi kesho Alhamis.

Mwili wa Marehemu Josephat Torner ukitolewa katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza leo Jumatano Aprili 15,2020 kwa ajili ya kusafarishwa kwenda wilayani Busega kwa ajili ya mazishi kesho Alhamis

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post