DC MBONEKO AKABIDHI MATENKI YALIYOTOLEWA NA MGODI WA BARRICK BUZWAGI KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA SHINYANGAMkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katikati, akimkabidhi Tenki la kuoshea mikono Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba (kushoto) .Wa kwanza kulia ni katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi. Matenki hayo yametolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ili kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katikati, akimkabidhi Tenki la kuoshea mikono Kaimu mk urugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mhe. Tito Kagize, wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi.Matenki hayo yametolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ili kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katikati, akipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukabidhi matenki ya kuoshea mikono katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na manispaa ya Shinyanga yaliyotolewa na Mgodi wa Barrick Buzwagi, kulia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba, na kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mhe. Tito Kagize.


Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amekabidhi Matanki ya kuoshea mikono ‘washing container’ yaliyotolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ili kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na manispaa ya Shinyanga.


Zoezi la kukabidhi matenki hayo mawili ya maji limefanyika  kwenye Ofisi za mkuu wa wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Aprili 27, 2020.

Mboneko amesema Tenki moja la maji katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga litawekwa kwenye hospitali ya wilaya iliyopo Iselamagazi na kwa upande wa  manispaa ya Shinyanga tenki la maji  litawekwa kwenye Stendi kuu ya Mabasi maeneo ambayo yana msongamono mkubwa wa watu.

“Nakabidhi matenki haya ya maji ambayo yametolewa na wadau wetu wa Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu Barrick kupitia mgodi wake wa Buzwagi, ambapo Tenki moja litakwenda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na jingine manispaa ya Shinyanga, lengo ni kuongeza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona,” amesema Mboneko.

“Naagiza pia Matenki haya ya maji yawekewe ulinzi wa kutosha na yasiharibiwe ili yadumu kwa muda mrefu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kunawa mikono kwa sabuni na maj itiririka, ili wasipate maambukizi ya virusi vya Corona na kubaki kuwa salama”,ameongeza.

Pia ametoa shukrani kwa wadau wote mkoani Shinyanga kwa kuendelea kuunga juhudi za Serikali kupambana na virusi vya Corona, na kutoa wito kwa wadau wengine waendelee kujitokeza kutoa msaada, ikiwa bado kuna maeneo mengi yana uhitaji wa vifaa ili wajikinge na virusi hivyo na kubaki salama.

Kwa upande wao wakurugenzi hao akiwemo Mhe. Hoja Mahiba wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mhe. Tito Kagize, wameahidi kuyalinda matenki hayo ya maji kwa kuweka ulinzi wa kutosha ili yasiharibiwe na kudumu muda mrefu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post