WAGONJWA WA CORONA TANZANIA WAFIKIA 13.....MGOJWA WA KWANZA KAPONA


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa corona  imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni Watanzania na watano ni wageni.


Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo Machi 26, 2020, wakati akitoa taarifa kwa umma, kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini

Amesema kati ya wagonjwa hao Dar es Salaam  wapo nane, Arusha wawili, Zanzibar wawili na Kagera mmoja.

Waziri Ummy amesema kuwa mgonjwa wa 13 alipatikana mkoani Kagera na ni dereva wa magari makubwa, ambaye aliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga na shughuli zake anafanyia kati ya Burundi, DRC na Tanzania. 


Pia amesema  mgonjwa wa kwanza nchini wa virusi vya corona, Isabela Mwampamba (46) ameshapona ugonjwa huo.“Mgonjwa wetu wa kwanza ambaye haturuhusiwi kutaja jina lakini alijitaja mwenyewe amepona COVID 19, tumepima sampuli mara tatu na zote zimeonyesha negative, tumeanza utaratibu wa kumruhusu kurudi nyumbani,” amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post