RAIS MAGUFULI : UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2020 HAUTAAHIRISHWA LICHA YA KUWEPO KWA CORONA


Rais John Magufuli amesema uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautaahirishwa licha ya kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya corona.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Machi 26,2020 Ikulu ya Chamwino, Dodoma wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ripoti ya Takukuru. 

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakifikiri kwamba kazi hazifanyiki na hakuna kukutana kwa sababu ya corona. Amesema hata nchi zilizoathirika zaidi na virusi hivyo, bado mabunge yao yanakutana kama kawaida. 

"Na uchaguzi tutafanya, wapo wanaofikiri kwamba tutaahirisha, nani anataka kukaa kwenye maofisi haya muda wote huo," amesema Rais Magufuli wakati akizungumza kwenye hafla ya kupokea ripoti hizo",amesema. 

"Kazi lazima iendelee kufanyika na uchaguzi tutafanya tu, wapo wengine wanafikiri nitaahirisha, ni nani anataka kukaa kwenye maofisi haya muda wote huu", ameongeza Rais Magufuli.

"Hatujazuiliwa kukutana, leo nimesoma gazeti moja linasema 'Madiwani wafanya kikao cha Madiwani', sijui alifikiri vikao vya madiwani vimezuiliwa kwa sababu ya Corona?. Sisi tunaendelea kukutana katika mikutano hii ya kawaida na hata Bunge ndiyo maana linaendelea", amesema Rais Magufuli.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527