Angalia Picha : DC MBONEKO AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA SHINYANGA...ATOA MAAGIZO MAZITO KAMPUNI ZA ULINZI

Jumla ya Vijana 141 wa wilaya ya Shinyanga Wamehitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba yaliyodumu kwa kipindi cha miezi kuanzia Novemba 4,2019 hadi Machi 10,2020.

Hafla ya Kufunga Mafunzo hayo imefanyika leo Jumanne Machi 10,2020 katika Viwanja vya Sabasaba katika kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya hiyo,amewataka wahitimu wa mafunzo kuonesha kwa vitendo uadilifu, uaminifu na uzalendo wao katika nchi.

Mboneko aliwataka askari hao ambao wanafanya kazi kwenye Makampuni mbalimbali kutojihusisha na vitendo vya uhalifu badala yake wawe mfano bora kuimarisha ulinzi katika jamii.

“Baada ya kumaliza mafunzo haya nina imani mtakwenda kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha vitendo viovu vinaisha kwenye maeneo yenu. Shirikianeni na Jeshi la polisi kuwabaini wahalifu na msaidie katika kuimarisha ulinzi katika jamii”,alisema Mboneko.

Mkuu huyo wa wilaya aliyaagiza Makampuni yote ya Ulinzi katika wilaya ya Shinyanga kuhakikisha yanakuwa na sare aina moja akieleza kuwa baadhi ya Makampuni ya Ulinzi yamekuwa na sare zaidi ya tatu.

“Nataka kila Kampuni ya Ulinzi itumie Walinzi waliopitia Mafunzo ya Jeshi la Akiba na kila Kampuni iwe na sare moja na ihakikishe inawapa mikataba ya ajira walinzi wake na kuwapatia mishahara kwa wakati”,alisema Mboneko.

Mboneko alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawaruhusu watoto wao kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Akiba.

Aidha aliyashukuru Makampuni mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd iliyochangia vinywaji baridi ‘soda na maji’ vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 300,000/= kufanikisha mafunzo hayo ya Jeshi la Akiba.

Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga,Kanali Justas Kitta aliwataka Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Akiba kuzingatia nidhamu,kuwa waaminifu na watiifu pamoja na kuwa nadhifu.

“Sitegemei kuona mhitimu anakamatwa na polisi kwa makosa mbalimbali,kuweni watiifu kwenye maeneo mliyoajiriwa na muwe wasafi”,alisema Kanali Kitta.

Akisoma Risala ya wahitimu, Recho Membo alisema walianza mafunzo hayo wakiwa 198 lakini waliofanikiwa kumaliza mafunzo hayo ni 141 kati yao wanaume ni 101 na wanawake 40.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali  Justas Kitta bila kugusana mikono wakati mkuu huyo wa wilaya akiwasili katika Viwanja vya Sabasaba Mjini Shinyanga kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Machi 10,2020 ambapo Jumla ya Vijana 141 wamehitimu mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 4,2020 hadi Machi 10,2020. Katikati ni  Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifurahia jambo na Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali  Justas Kitta (kulia) na Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege (katikati) alipowasili katika Viwanja vya Sabasaba Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Jumanne Machi 10,2020 Viwanja vya Sabasaba Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo Jumla ya Vijana 141 kutoka wilaya ya Shinyanga wamehitimu mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 4,2019.

Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali  Justas Kitta akizungumza wakati hafla ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Jumanne Machi 10,2020 Viwanja vya Sabasaba Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo Jumla ya Vijana 141 kutoka wilaya ya Shinyanga wamehitimu mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 4,2019.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiteta jambo Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga,Kanali Justas Kitta (wa pili kushoto) na Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege (kulia). Wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamanda wa JWTZ Kikosi cha 82 Old Shinyanga,  Meja Saleh Ally.

 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipokea Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakiwa kwenye Paredi wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiongozana na Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege kukagua Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikagua Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akielekea kuketi baada ya kukagua Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege akielekea kuketi baada ya kukagua Paredi ya Vijana kutoka wilaya ya Shinyanga waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa amekaa na  Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali Justas Kitta (wa pili kushoto) na Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege (kulia). Wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamanda wa JWTZ Kikosi cha 82 Old Shinyanga,  Meja Saleh Ally na Kamanda wa JWTZ Kikosi cha 516 Kizumbi, Meja Benard Emmanuel kwenye Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum akiwa kwenye hafla ya Kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba leo Machi 10,2020.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) na Viongozi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa mwendo wa polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wakitembea kwa wa haraka mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

MC wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba, Sajenti Isaya Mbise (kushoto) akiwa na Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Sajenti Geofrey Kamala.
Recho Membo akisoma risala ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba.
Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakiimba shairi.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakitoa burudani.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakionesha mchezo wa  singe.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakitoa burudani uwanjani.
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakicheza kwaito.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum akimkabidhi Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Sajenti Geofrey Kamala zawadi ya fedha kwa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga waliotoa burudani kwenye hafla ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko. Ili kufanikisha hafla hiyo, Kampuni ya Jambo pia ilichangia vinywaji baridi vyenye thamani ya Shilingi 300,000/=.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Sajenti Geofrey Kamala akigawa zawadi ya fedha zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum kwa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga waliotoa burudani kwenye hafla ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali  Justas Kitta wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba. 
Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege  akisoma taarifa ya Mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga.
Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege  akisoma taarifa ya Mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akikabidhi zawadi ya fedha kwa Mhitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba, Shauri Benjamini aliyefanya vizuri upande wa kwata wakati wa mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akikabidhi zawadi ya fedha kwa Mhitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba, Meshack Nestory aliyefanya vizuri upande wa darasani wakati wa mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akikabidhi zawadi ya fedha kwa Mhitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba, Ally Tumbwe aliyefanya vizuri upande wa kutumia silaha wakati wa mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akikabidhi zawadi ya fedha kwa Mhitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba, Sarah Stephen aliyefanya vizuri upande wa Nidhamu wakati wa mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akikabidhi zawadi ya fedha kwa Mhitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba, Tano Lusana aliyefanya vizuri upande wa upigaji shabaha wakati wa mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi zawadi ya fedha kwa Mhitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba, Balasta Benard aliyefanya vizuri upande wa  porini wakati wa mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga waliopata zawadi za ushindi kwa kufanya vizuri wakati wa mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali yaliyofanikisha mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali  Justas Kitta (kushoto) na Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege (kulia).

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali  Justas Kitta ( wa pili kushoto),Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga, Meja Ford Mwakasege (kulia) na Wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamanda wa JWTZ Kikosi cha 82 Old Shinyanga,  Meja Saleh Ally ( wa kwanza kushoto).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na Maafisa watendaji wa kata.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na Wakufunzi wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527