Picha : WANANCHI SHINYANGA WAJITOKEZA KWA WINGI KUUAGA MWILI WA MZEE KANUMBA...KUZIKWA KESHO SIMIYU
Wananchi wa Shinyanga wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa Baba mzazi wa msaani wa Bongo Movies marehemu Stephen Kanumba, mzee Charles Kanumba (71)  kwa ajili ya kesho kusafirishwa kwenda katika kijiji cha Nyakaboja Busega  mkoani Simiyu kumpumzisha kwenye makazi yake ya milele.

Zoezi la kuuga mwili huo wa marehemu mzee Charles Kanumba, limefanyika leo Jumanne Machi 10,2020 nyumbani kwake katika mtaa wa Magadula Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, huku ibada hiyo ya kumuaga ikiongozwa na mchungaji Benjamini Makaranga wa kanisa la AICT Ngokolo.

Akisoma historia ya marehemu kwa niaba ya familia Lubeni Zakayo, ambaye ni ndugu wa karibu na familia ya marehemu mzee Charles Kanumba, alisema marehemu alizaliwa mwaka 1949 huko Busega mkoani Simiyu.

Alisema mara baada ya kustaafu kazi Serikalini mwaka 2015, ndipo mwaka huo alipoanza kusumbuliwa na maradhi ya nyonga, tumbo, magoti, pamoja na kibofu cha mkojo, hadi umauti ulipomkuta Machi 8 mwaka huu, na kesho watazika mwili wa marehemu nyumbani kwao katika kijiji cha Nyakaboja Busega  mkoani Simiyu.

Aliongeza marehemu ameacha mjane pamoja na watoto Saba, ambapo alifanikiwa kuzaa watoto Tisa, lakini wawili wameshatangulia mbele za haki, watoto wa kiume Watano na wa kike wanne.

Kwa upande wake mchungaji Zabroni Mang’wenghula kutoka Kanisa la AICT Ndala, aliwataka wananchi kumtumaini mungu katika enzi za uhai wao, ili kujiweka tayari pindi watakapotwaliwa na bwana.


TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

Mwili wa marehemu mzee Charles Kanumba ukiwa ndani ya Jeneza leo Jumanne Machi 10,2020. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog


Mwili wa marehemu Charles Kanumba ukiwa ndani ya Jeneza kwa ajili ya wananchi kuuga mwili wake ambapo kesho utasafirishwa kwenda kuzikwa huko Busega Mkoani Simiyu.

Mke wa marehemu, Rehema Ramadhani, akimuaga mme wake ambaye atasafirishwa kesho kwenda kuzikwa huko Busega Simiyu.

Ndugu wakiendelea kuaga mwili wa marehemu.

Mwili wa marehemu Charles Kanumba ukiwa ndani ya Jeneza kwa ajili ya wananchi kuuga mwili wake ambapo kesho utasafirishwa kwenda kuzikwa huko Busega Mkoani Simiyu.

Mke wa marehemu mzee Charles Kanumba, Rehema Ramadhani, mwenye nguo Nyeupe akiwa kwenye msiba wa mmewake.

Mchungaji Benjamini Makaranga wa kanisa la AICT Ngokolo akiongoza Ibada kumuaga marehemu mzee Charles Kanumba.

Ndugu wa karibu na familia ya marehemu Lubeni Zakayo, akisoma risala ya marehemu.


Wananchi wakiwa kwenye msiba wa marehemu mzee Charles Kanumba nyumbani kwake katika mtaa wa Magadula Kata ya Ngokolo.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post