HARMONIZE FEKI ACHEZEA KICHAPO KUTONGOZA HOVYO INSTAGRAM



Picha ya Harmonize feki
Moja kati ya video inayozunguka kwa sasa mitandaoni, inamuonesha jamaa mmoja akichezea kichapo kutoka kwa mwanamke aliyemdanganya kuwa yeye ni Harmonize wakati sio kweli ili mradi awe naye kwenye mahusiano.

Jamaa huyo ambaye jina lake halijajulikana, amechezea kichapo hicho mbele ya waandishi wa habari huku mwanamke huyo akiwa amemkunja shingoni, huku akimuuliza kwanini amemdanganya kuwa yeye ni Harmonize katika mtandao wa Instagram.

Katika utetezi wa jamaa huyo alisikika akisema "Muonekano ni kama hivi unavyouona ni fresh tu, mimi nafanana na Harmonize sijifananishi bali nafananishwa na watu au sio ila nampenda sana".

Aidha wakati huo mwanamke huyo alikuwa anampiga kichwani huku amemkunja na kumuuliza "Kwanza usiniguse wewe una Corona, ongea vizuri kwanini umeamua kunidanganya wewe ni Harmonize na ukanitongoza Instagram".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527