TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) WAKUTANA NA VYAMA VYA SIASA KUJADILI KUHUSU UCHAGUZI MKUU


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutana na viongozi wa vyama vya siasa kwa lengo la kuzungumzia masuala ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.


Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) nchini Tanzania, Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa uboreshaji wa awamu hii kama ulivyokuwa ule wa mara ya kwanza utawahusu wapiga kura wapya ambao ni raia wa watanzania waliotimiza miaka 18 au watatimiza umri huo siku ya Uchaguzi Mkuu, zoezi hili pia litawahusu wale wanaoboresha taarifa zao mathalani walihama kutoka maeneo yao ya awali na kuhamia maeneo mengine yakiuchaguzi na wale ambao kadi zao zimeharibika au kupotea.

Aidha amesema kuwa zoezi hilo pia litawahusisha kuwaondoa kwenye daftari wapiga kura waliofariki na wengine waliopoteza sifa kwa mujibu wa sheria


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527