AMUUA MPENZI WAKE GESTI KISHA KUJIKATA KOROMEOKamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Ulrich Matei.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Festo Maduhu, Mkazi wa Mtaa wa Benki Kabwe Jijini Mbeya kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake na kisha yeye mwenyewe kujaribu kujiua kwa kisu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 22, 2020 na Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ulrich Matei ambapo amesema tukio hilo limetokea jana, huku kiini cha tukio hilo kikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi, ambapo Maduhu alikuwa akimtuhumu mwenzake kuwa ana mahusiano na mwanaume mwingine.

"Ni kwamba Machi 23, 2020, majira ya saa 09:00 asubuhi, huko katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Negero, iliyopo Mtaa wa Ilolo, Kata ya Ruanda, katika chumba namba 111, mwanamke mmoja aitwaye Jesca Michael, Mhudumu wa nyumba ya kulala wageni na bar, aligundulika kuuawa kwa kukabwa shingo na kupigwa sehemu za usoni na mtuhumiwa Festo Maduhu ambaye ni mpenzi wake" imeeleza taarifa hiyo.

Katika ufuatiliaji wa kumkamata mtuhumiwa mara baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alikutwa akiwa amejifungia nyumbani kwake na baada ya Askari kuvunja mlango wa nyumba hiyo, alikutwa akiwa anaendelea kujichinja koromeo lake kwa kutumia kisu ambapo Askari Polisi walimuokoa na kumpeleka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post