ASILIMIA 39 YA WANAWAKE WALIOPO KWENYE NDOA,WAMEFANYIWA VITENDO VYA UKATILI

Na John Walter-Manyara
Takwimu nchini Tanzania zinaonyesha asilimia 49 ya wanawake wamefanyiwa vitendo vya Ukatili huku nusu ya Wanawake walioolewa,asilimia 39 wamefanyiwa vitendo hivyo.


Hayo yamebainishwa na Mwakililishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Hanifa Selenga, akizungumza katika sherehe za Maazimisho ya siku ya Wanawake  Machi 5 mjini Babati.

Kwa upande mwingine Katika kusheherekea Wiki ya Mwanamke duniani,nchini Tanzania  wanawake wameandaa Msafara Wa kijinsia kutokomeza Ukatili,twende pamoja ukihimiza kupewa haki ya usawa katika kumiliki ardhi kwa wanawake.

Hanifa amesema lengo la Msafara huo ni kueneza ujumbe wa kukemea vitendo vya Kikatili katika jamii.

Kauli mbiu inayoongoza maazimisho hayo kwa mwaka 2020 inasisitiza Kizazi cha Usawa Wa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na Baadae.

Pamoja na mambo mengine,katika wiki hii wanawake wanaojishughulisha na ujasiriamali wanapata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa wanazozizalisha.

Amesema wamepita mikoa ya Kusini,Kaskazini na kwa sasa baada ya Manyara, wanaelekea mkoani Mwanzan na hatimaye wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwenye kilele cha Maazimisho hayo ambapo mgeni Rasmi atakuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post