Breaking : WAZIRI MKUU FREDRICK SUMAYE ATANGAZA KURUDI CCM



Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye leo ametangaza kurudi tena Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kikao cha Baraza la Wadhamini, Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba - Dar es salaam.

Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye ametangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka CHADEMA kupokelewa na Katibu mkuu Wa Chama hicho Dkt.Bashiru Ally leo Jumatatu Februari 10,2020 katika ofisi ndogo za chama hicho tawala nchini Tanzania zilizopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye n Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa (Waliohama CCM na kuhamia CHADEMA na wamerudi tena CCM).
Sumaye ametangaza uamuzi wa Kurejea CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally katika kikao cha baraza la wadhamini kilichoanza leo asubuhi.

Sumaye amerejea CCM takribani miezi miwili tangu alipotangaza kuwa si mwanachama wa Chadema.

Desemba 4, 2019 Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu mwaka 1995 hadi 2005 katika Serikali ya Awamu ya Tatu, alijivua uanachama wa Chadema na kumuachia ujumbe mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe.

Alijiondoa Chadema siku chache baada ya kupigiwa kura 48 za hapana kati ya 76 katika uchaguzi wa uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

Sumaye alieleza kuwa kutokana na yaliyotokea kwenye uchaguzi huo na yeye kuchukua fomu ya kuwania uenyekiti wa Chadema akipambana na Mbowe haoni haja ya kubaki katika chama hicho.

Sumaye alikuwa Waziri Mkuu wa zamani wa pili kujiondoa chama tawala katika historia ya Tanzania, ambapo waziri mkuu wa kwanza kuhama CCM na kujiunga na Chadema alikuwa Edward Lowassa, aliyefanya hivyo mwaka 2015. Hata hivyo, Machi Mosi, 2019 Lowassa alirejea CCM.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527