ESRF YAENDESHA KONGAMANO LA KILIMO BIASHARA


 Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi kwa washiriki wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.


 Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Magreth Nzuki akizungumzia malengo ya warsha kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtafiti mshiriki mwandamizi kutoka ESRF, Dr Oswald Mashindano akizungumzia fursa za kilimo kwenye miji na fursa za uwekezaji kama zilivyoainishwa kwenye miongozi ya uwekezaji kwenye mikoa mbalimbali wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Umoja wa Vijana Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS), Bw. Philemon Kiemi akitoa mada kuhusu ufugaji wa kisasa wa nyuki wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu kutoka SUA, Ltn Joseph Lyakurwa akitoa mada kuhusu ufugaji wa Samaki katika matanki kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dr. Hieromin Lamtane akitoa mada kuhusu malisho ya chakula cha samaki kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu kutoka Agriculture Media, Bw. Raphael Majivu akitoa mada kuhusu kilimo cha malisho ya mifugo bila udongo (Hydroponic Fodder) pamoja na kilimo cha Azola (Chakula cha mifugo na mbolea) wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akijadiliana jambo na Meneja wa Data wa ESRF, John Kajiba (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Magreth Nzuki wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakipata maelezo ndani ya kitalu maalum kuhusu kilimo cha mbogamboga bila kutumia udongo wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu kutoka SUA, Ltn Joseph Lyakurwa akitoa maelezo kwa vitendo kwa washiriki kuhusu ufugaji wa Samaki katika matanki wakati wa warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha ya fursa katika kilimo biashara iliyofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
***
TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), imeendesha kongamano kubwa la fursa za kilimo biashara kwa lengo kuhimiza matumizi ya teknolojia ili kuboresha tija katika sekta ya kilimo.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ESRF Bi. Margareth Nzuki alisema, Taasisi hiyo ikishirikiana na Serikali kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) limekuwa likifanya tafiti mbalimbali ili kuainisha fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali ya uchumi. 

Ameongeza kuwa kwa ufadhili wa UNDP,  ESRF ikishirikiana na Serikali za Mikoa limefanya  utafiti kuainisha  fursa mbalimbali za uwekezaji katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na mpaka sasa imekwisha kamilisha kutayarisha Miongozo ya Uwekezaji wa Mikoa 15 na inaendelea kumalizia mikoa mingine iliyobaki. Amesema  katika miongozo hiyo fursa nyingi zinatoka katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji.

Bi Nzuki amewaambia washikiri kuwa lengo la Kongamamo hilo ni kushirikishana na kutoa maarifa mapya katika kilimo biashara.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema  kukua kwa teknolojia duniani kumeongeza fursa nyingi na kuwezesha wakulima katika sehemu mbalimbali duniani kutokutegemea mvua.

"Teknolojia imewezesha wakulima kutumia eneo dogo la ardhi kuzalisha kiwango kikubwa cha mavuno ya mazao yaliyo bora; teknolojia pia imewezesha wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo cha kisasa toka kwa wataalamu kwa haraka na muda muafaka, hivyo kusaidia kupata mavuno mengi na bora," alisema Dk. Kida.

Kilimo hicho cha kutegemea teknolojia za kisasa kinachoitwa kwa kiingereza “Smart Farming Agriculture” ambacho hakihitaji maeneo makubwa ya ardhi na kinaweza pia kufanyika katika miji.

Uwingi na ubora wa mazao yanayozalishwa ni kiashiria cha fursa ya kufanya biashara kwa tija, kwa sababu mazao hayo yatamvutia mnunuzi na yanaweza kuuzwa popote duniani kutokana na sifa zake za ubora; mfano kwenye maduka makubwa na mahotelini ambako wateja wengi katika zama hizi wanapenda vyakula vya asili ambavyo havina kemikali ambayo inatumika kukuzia mimea mashambani.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ajili ya wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wengine katika sekta ya Kilimo.
kwa mujibu wa Dk. Kida wakufunzi mbalimbali waliobobea na wanaojihusisha katika fani mbalimbali za Kilimo biashara wametarajiwa kutoa uwelewa kwa kuwajengea uwezo washiriki ili kutafuta utatuzi wa vikwazo mbalimbali ambavyo wakulima na wafugaji mmekuwa mnakabiliana navyo.

Katika kongamano hilo lililofanyika mwishoni mwa juma mada zilizofundishwa naa kujadiliwa Kwa kina ni pamoja na:malisho ya chakula cha samaki,ufugaji wa samaki katika matanki (Recirculating Aquaculture System), kilimo cha mboga mboga bila kutumia udongo (Hydroponic Vegetable),kilimo cha azolla kwa ajili ya malisho ya mifugo na mbolea, ufugaji wa kisasa wa samaki kwa kutumia vizimba, matanki na mabwawa,ufugaji wa kisasa wa nyuki na kubadilishana uzoefu katika kilimo biashara.

Washiriki wengine pamoja na wakulima na wafugaji ni taasisi za fedha nchini za TADB, CRDB, SELF na PASS Trust.
Wadau hao hutumiwa na wadau wengi katika kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya mtu mojammoja, vikundi  na Taifa kwa ujumla.  

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post