PROFESA LIPUMBA AMUOMBA RAIS MAGUFULI AKUTANE NA WAPINZANI KABLA YA UCHAGUZI MKUU


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amemshauri Rais Magufuli kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kubadilishana mawazo na kujadili masuala mbalimbali ikiwamo Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Profesa Lipumba metoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 10, katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine pia amemshauri kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ili kuviruhusu vyama kueneza sera zake kwa wananchi.

“Sheria ya vyama vya siasa inataka kila chama kuwa na rejesta, lakini utekelezaji wa kipengele hicho unahitaji kuhamasisha wananchi.

“Kwa hiyo tunapohitaji mikutano ya hadhara si tu kueneza sera, pia tunataka kutekeleza mara kwa ya Sheria ya vyama vya siasa,” amesema Profesa Lipumba.

Kuhusu CUF kusimamisha wagombea, amesema Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho limeshaamua kuwa litasimamisha wagombea katika ngazi zote Tanzania Baraza na Visiwani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527