MUME AMUUA MKEWE KWA MKUKI TABORA

Hawa Juma mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Kijiji cha Isikizya wilayani Uyui mkoani Tabora ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kinachodaiwa kuwa ni mkuki na mumewe Omari Mkuyu alipokuwa amelala.

Mauaji ya mwanamke huyo yametokea usiku wa kuamkia Februari 25 mwaka huu baada ya kuibuka mzozo baina ya wanandoa hao unaohusishwa na wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Barnabas Mwakalukwa amethibitisha tukio hilo la kinyama kutokea na kuongeza kuwa mtuhumiwa tayari anashikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527