RC MTWARA KUKUTANA NA WATENGENEZAJI WA GONGO ILI KUJADILI NAMNA YA KUIBORESHA


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema bado nia yake ya kukutana na Watengenezaji wa pombe aina ya gongo iko palepale.

Amesema, lengo ni kujadiliana na kuona namna nzuri ya kuiboresha pombe hiyo kwa kuipelekea TBS na kwa Mkemia ili ipimwe na kuondoa sumu

Amesema, badala ya kuikuza na kuona kuwa hapa kuna kitu kinaweza kutupeleka kwenye viwanda, tunazuia. Je, mnaokunywa hizo pombe za viwandani mnajua asili yake?

Amehoji, "Kwanini gongo haitambuliwi kama kinywaji halisi cha Kitanzania?" Na kusisitiza kuwa atakutana na Watengenezaji wa gongo ili waone namna ya kuiboresha

Amesema “Nasisitiza nitakutana na watengenezaji wa gongo, kama unamfahamu mwambie aje tuzungumze jinsi ya kuiboresha zaidi na ituletee faida, hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda ya zuiazuia, tunapaswa kuwa na Tanzania ya Viwanda ya wezeshawezesha"

Itakumbukwa kuwa Katika Mkutano wa 11, Kikao cha 4 cha Bunge la Aprili 11, 2008, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge alisema yawezekana kabisa tuna pombe kali zaidi ya gongo, la msingi lililozingatiwa katika kupiga marufuku pombe aina ya gongo ni kwa sababu njia inayotumika kutengenezea si ambayo inazingatia usafi na afya ya binadamu, ndiyo maana imekuwa ni haramu kwa mujibu wa sheria.

Pale ambapo viwanda vya kutengeneza pombe ambayo inakubalika kwa masharti ya afya ya binafamu, vitakapoanza kutengeneza gongo, ndiyo hapo ambapo tutazingatia kuihalalisha pombe hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527