Iran Yasema Ina Jeshi Imara la Anga Licha ya Mashinikizo na Vikwazo Vya Marekani

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema leo kuwa jeshi la anga la Iran ni madhubuti licha ya vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo na Marekani tangu mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979. 

Khamenei ametoa matamshi hayo wakati alipozungumza na makamanda pamoja na wafanyakazi wa jeshi la anga la Iran.

Kulingana na shirika la habari la serikali nchini humo IRNA, Khamenei amesema tangu mapinduzi ya kiislamu, lengo la Marekani limekuwa kuwazuia kuwa na jeshi thabiti la la anga hali sivyo ilivyo. 

Iran inaadhimisha miaka 41 ya mapinduzi ya kiislamu yaliooiondoa mamlakani serikali ya Shah Mohammad Reza Pahlavi iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani.

Taifa hilo la kiislamu, limeaapa kuimarisha uwezo wake wa kijeshi licha ya shinikizo kutoka kwa mataifa ya Magharibi ya kutaka kukatiza uwezo wake wa kijeshi ikiwa ni pamoja na mpango wake wa makombora.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post