IDADI YA WALIOFARIKI KWA VIRUSI VYA CORONA CHINA YAFIKA WATU 811


Idadi ya waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini China imeongezeka kwa vifo 89 na kufikia watu 811. 


Mmarekani na Mjapani pia ni miongoni mwa waliokufa. Watu hao ni raia wa kwanza wa kigeni kufa tangu kuzuka kwa mripuko huo.

 Shirika la afya duniani limesema kumekuwa na jumla ya maambukizi 34,800 duniani kote. 

Eneo lililoathirika zaidi ni China Bara, ambako kumethibitishwa watu 34,546 walioambukizwa.

 Raia watano wa Uingereza akiwemo mtoto wamegundulika kuwa na virusi hivyo nchini Ufaransa.

 Waziri wa Afya wa Ufaransa Agnes Buzyn amesema raia hayo waliambukizwa na raia mwingine wa Uingereza ambae katika siku za hivi karibuni alikuwa nchini Singapore.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post