ERICK KABENDERA AACHIWA HURU KWA MASHARTI YA KULIPA FIDIA AU KIFUNGO CHA MIEZI 3 | MALUNDE 1 BLOG

Monday, February 24, 2020

ERICK KABENDERA AACHIWA HURU KWA MASHARTI YA KULIPA FIDIA AU KIFUNGO CHA MIEZI 3

  Malunde       Monday, February 24, 2020

Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera amehukumiwa kulipa faini Sh100 milioni baada kukiri kosa la  utakatishaji fedha na pia kulipa faini ya Sh250,000 au kwenda jela miezi mitatu kwa kukiri kukwepa kodi,pamoja na fidia ya shilingi milioni 172. 

Mapema leo, Kabendera aliyekuwa akikabiliwa na makosa matatu, alifutiwa kosa lake alilokuwa akidaiwa Kuongoza Genge la Uhalifu.


Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya Kabendera kusota korokoroni tangu alipofikishwa mahakamani hapo Agosti 5, 2019.

Kabendera anatakiwa kulipa kiasi cha Sh.Mil 173 ndani ya miezi 6, huku kiasi cha Sh.Mil 100 akiwa tayari ameshaingiza katika akaunti ya Serikali.

Kabendera kwa sasa yupo huru, huku akitakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post