MWANDISHI WA HABARI , ERICK KABENDERA ATIWA HATIANI KWA MASHITAKA MAWILI


Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani mwandishi wa habari , Erick Kabendera.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo Jumatatu Februari 24, 2020 baada ya Kabendera kukiri mashtaka yake mawili ya kukwepa kodi na kutakatisha Sh173 milioni.

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya upande wa mashtaka kumsomea maelezo ya awali ya mshtakiwa huyo.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu

Leo amefutiwa shtaka la kuongoza genge la uhalifu na kubaki na mashtaka mawili ya kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 milioni.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527