WATU WASIOJULIKANA WAIBA VIFAA VYA NIDA ARUSHA


Watu wasiojulikana wameiba mashine zote za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) zilizokuwa katika kituo kidogo cha NIDA katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo, kituo hicho kimefungwa kwa leo na Polisi wameanza mchakato wa kuwasaka waliohusika na wizi huo.Mkuu wa wilaya Arumeru, Jerry Muro amesema wizi huo umetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Januari 6, 2020 katika ofisi za Nida zilizopo jengo la halmashauri ya Wilaya ya Arusha (DC).

Muro amesema vifaa vilivyoibwa ni kamera mbili, stendi mbili, kompyuta mpakato mbili, kompyuta moja (Desk top), stendi mbili, Extation mbili, keyboad moja na Damalog moja.

"Vifaa vyote vimeibiwa, tumepata mshtuko, milango haikuvunjwa inaonekana ni wizi wa kimkakati umefanywa ndani, vifaa vya NIDA ni mali za Taifa sasa hawa wanapata wapi ujasiri wa kuiba!"- Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya Arumeru


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post