MO DEWJI AJIUZULU SIMBA SC,NI BAADA YA KUPOTEZA FAINALI YA JANA


Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC MO Dewji amefikia maamuzi mazito ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti na kubakia kama muwekezaji wa Simba.MO amefikia hatua hiyo kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakitolewa na UD Songo ya Msumbiji hatua ya awali, sare ya 2-2 dhidi ya Yanga inayoonekana kupitia kipindi kigumu kiuchumi na kupoteza fainali ya jana ya Mapinduzi Cup 1-0 dhidi ya Mtibwa.


“Ni aibu Simba kutoshinda, baada ya kulipa mishahara inayokaribia Bilioni 4 kwa mwaka, najiuzulu kama mwenyekiti wa bodi na kubakia muwekezaji, Simba Nguvu Moja, nitatia nguvu kwenye kuendeleza miundombinu na soka la vijana” Ameandika MODewj
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post