ALIYEKUWA KIONGOZI WA BRIGEDI YA FARU APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA JESHI NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TABORA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, January 14, 2020

ALIYEKUWA KIONGOZI WA BRIGEDI YA FARU APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA JESHI NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TABORA

  Malunde       Tuesday, January 14, 2020

NA TIGANYA VINCENT
Aliyekuwa Kiongozi   wa Brigedi ya Faru amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Jeshi la Wananchi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi.


Kauli hiyo imetolewa  na aliyekuwa kiongozi katika Brigedi ya Faru ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti wakati wa mazungumzo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alipofika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa tabora kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhama Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma.


Alisema katika kipindi alipokuwa akisimamia Brigedi ya Faru, Jeshi la Wananchi limeweza kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira na upandaji miti katika kutekeleza agizo la Makamu wa Rais.

Brigedia Jenerali Sibuti aliongeza kuwa ana matumaini Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi yake ya kuongoza Brigedi ya Faru ataendelea ushirikiano uliopo na kuchochea maendeleo ya eneo hilo.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alimshukuru Brigedia Jenerali Sibuti kwa mchango wake mkubwa wa kukuza ushirikiano kati ya Jeshi la Wananchi na Mkoa wa Tabora na kusaidia katika upandaji miti kwa kutumia wanajeshi.

Naye Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru alisema Jeshi la Wananchi litaendelea kuunga mkono juhudi za uongozi wa Ofisi ya Mkoa wa Tabora ya kuugeuza Mkoa huo kuwa wa kijani kwa ajili ya kukabiliana na uharibifu wa mistu.

Alisema ataendelea kutoa Vijana wa Jeshi la Wananchi ili waweze kushiriki katika upandaji wa miti na shughuli nyingine za maendeleo kwa ustawi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru akifafanua jambo wakati alipomsindikiza  aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru, Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (katikati) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhamia Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma. Wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kulia)  na pembeni ni Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Tabora Kanali Mussa Luka Simengwa.

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (aliyesimama) akitoa maelezo mafupi mara baada ya kukutana na aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (katikati) ambaye alifika katika  kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhamishiwa Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma. Wengine ni Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru na aliyepembeni ni Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Tabora Kanali Mussa Luka Simengwa. 

Aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru na kuhamia Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (wa pili kutoka kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (wa tatu kutoka kushoto) , Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru(katikati) wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Maafisa wa Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumalizika mazungumzo ya aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru Bregedia Jenerali  Sibuti kuagana na uongozi wa Mkoa wa Tabora .


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post