Marekani Yasema Iko Tayari Kufanya Mazungumzo na Iran Bila Masharti Yoyote | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, January 9, 2020

Marekani Yasema Iko Tayari Kufanya Mazungumzo na Iran Bila Masharti Yoyote

  Malunde       Thursday, January 9, 2020
Serikali ya Marekani imetangaza kuwa, iko tayari kufanya mazungumzo na Iran bila masharti yoyote.

Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa,  balozi na mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Kelly Craft  ametangaza katika umoja huo kwamba, nchi yake ipo tayari kuanza mazungumzo na Iran bila masharti yoyote.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Rais wa Marekani Donald akizungumza jana katika hotuba yake kuhusiana na mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya kambi za kijeshi za nchi hiyo nchini Iraq alidai kuwa, hakuna raia wa Iraq au Marekani aliyeuawa katika shambulio hilo japo kambi hizo ziliharibiwa kidogo. 

Trump alidai kwamba, Iran inaonekana kurudi nyuma, hatua ambayo ni nzuri kwa pande zote husika. Hata hivyo alisema kuwa, ataongeza vikwazo dhidi ya Iran.

Wakati Rais Trump akidai kwamba, hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa au kuuawa katika shambulio hilo, vyombo vya Iran jana vilisema kuwa Wanajeshi 80 wa Marekani  waliuawa japo havikutoa uthibitisho wowote


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post