MVULANA WA MIAKA 10 AJITAHIRI KWA KISU AKIOGOPA KUCHEKWA NA WENZIE


Mvulana wa miaka 10 mkazi wa kijiji ya Itare nchini Kenya amejitahiri kwa kutumia kisu cha jikoni baada ya wazazi wake kushindwa kulipia gharama ya Ksh 1000/- ya kupewa huduma hiyo hospitali.

Mtoto huyo wa darasa la pili ameeleza chombo cha habari kimoja nchini humo kuwa alilazimika kufanya hivyo kwa kuhofia unyanyapaa atakaofanyiwa na wenzake ambao wao walifanyiwa toraha kipindi cha likizo ya mwezi Desemba.

Inaelezwa kuwa hali ya mtoto huyo kiafya sio nzuri tangu alipojifanyia kitendo hicho mwezi mmoja uliopita na awali alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kisii lakini wazazi wake walimrudisha nyumbani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Mwanaharakati wilayani Kisii, Samwel Momanyi ameomba serikali iingilie kati na kumsaidia mtoto huyo kupata matibabu kwani anapata maumivu makali sana hususani akijisaidia haja ndogo.

Mvulana huyo ameshindwa kuanza masomo shule zilivyofunguliwa  siku ya Jumatatu Januari 6,2020 kutokana na afya yake kutoimarika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527