MAREKANI YAJIANDAA NA SHAMBULIZI LA KULIPIZA KISASI KUTOKA IRAN... WANAJESHI WENGINE 3500 KUTUMWA MASHARIKI YA KATI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, January 5, 2020

MAREKANI YAJIANDAA NA SHAMBULIZI LA KULIPIZA KISASI KUTOKA IRAN... WANAJESHI WENGINE 3500 KUTUMWA MASHARIKI YA KATI

  Malunde       Sunday, January 5, 2020

Marekani kwa sasa inajiandaa na shambulizi la kulipiza kisasi kutoka Iran baada ya shambulizi lake la anga kumuua kamanda mkuu wa Iran, hatua ambayo imetia wasiwasi nchi zote duniani na hata kutiliwa shaka na baadhi ya wabunge wa Marekani.

Shambulizi la anga la Marekani Alhamis lilimuua Meja Jenerali Qassem Soleiman, mkuu wa kikosi cha Quds, pamoja na kamanda wa wanamgambo wa Iraq, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, na kuchochea vitisho vikali vya kulipiza kisasi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.

Ikijibu tishio hilo linalozidi kuongezeka dhidi ya wafanyakazi na vituo vya Marekani katika Mashariki ya Kati, wizara ya ulinzi ya Marekani imetoa taarifa ikisema itasambaza kikosi huko Kuwait kama hatua ya tahadhari na sahihi, bila kutaja idadi ya wanajeshi. 


Hata hivyo vyombo vya habari vya Marekani jana vilitangaza kuwa nchi hiyo itatuma zaidi ya askari 3,500 wikiendi hii. Na askari wengine wa ziada kutoka divisheni ya 82 ya askari wa parashuti watapelekwa Iraq, Kuwait na sehemu nyingine za kanda hiyo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post